22 Machi 2019 - 08:54
Trump ataka Milima ya Golan itambuliwe kuwa ya Israel

: Rais wa Marekani Donald Trump amesema ni wakati sasa wa kutambua Milima ya Golan ambayo ni mali ya Syria, kuwa sehemu ya Israel

Shirika la habari la ABNA: Rais wa Marekani Donald Trump amesema ni wakati sasa wa kutambua Milima ya Golan ambayo ni mali ya Syria, kuwa sehemu ya Israel akisema eneo hilo ni muhimu kwa utulivu wa kikanda. Wito huo wa Trump alouandika kwenye ukurasa wa Twitter, umekuja wakati Waziri wake wa Mambo ya Kigeni Mike Pompeo akikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem. Israel ilichukua udhibiti wa thuluthi mbili ya upande wa magharibi wa Milima ya Golan, ambayo kihalisia ni sehemu ya Syria, wakati wa Vita vilivyodumu Siku Sita katika mwaka wa 1967. Sehemu ya mashariki ya Golan inasalia chini ya udhibiti wa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria. Upande wa Magharibi wa Golan ulioendelea kukaliwa jeshi la Syria kuanzia 1967 hadi 1981 wakati serikali ya Israel kimsingi ilipolichukua eneo hilo. Ujumbe huo wa Trump umekuja wakati Netanyahu akipambana vikali kuchaguliwa tena. Utawala wa Trump unamuunga mkono wazi Netanyahu, ambaye pia yuko chini ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa, kabla ya uchaguzi huo wa Aprili 9. Maamuzi haya yanakuja baada ya mpango wa Marekani wa kuigawanya mashariki ya kati kufeli.

Kwa upande wa Syria wamesisitiza kuwa Golan ni sehem yao na itabaki kuwa yao, na ikibidi wataichukua kwa nguvu za kijeshi.

Mwisho wa habari / 291